MWANAMKE FAHAMU NAFASI ULIYO NAYO KWA MWANAUME UJITENGE NA KUTUMIKA KAMA DARAJA KWENYE MAHUSIANO/NDOA
Ni kweli kabisa;-


Shida ipo kwenye nani anapashwa kupewa nafasi ya kumiliki moyo wa Mwingine, Maana kwa sasa MAHUSIANO mengi yanaanzia kwenye MITEGO YA VITU kwamba kama una kitu ni rahisi kupata upendeleo hata kama huna MVUTO



Wanawake wamekuwa wakililia UPENDO kiasi kwamba wakagundua siraha pekee ya kupata UPENDO WA MWANAUME NI KUMILIKI PESA hapo ni rahisi kuchagua kama mbuzi zizini ni yupi aliyenonaaaa

Naongea na wewe Mwanamke;-


Maana mwanaume kama hana pesa hawezi kuwazia MAPENZI kwani mihemko ya Mwanaume hutokana na AMANI ya KIPATO chake mwenyewe, Sasa ukampe pesa ili apate AMANI ili mihemko ipande kwa Mwanamke Mwingine ndo uje kukoma, Maana fahari ya Mwanaume ni kumhudumia Mwanamke aliye mchagua mwenyewe, Kwani hela yako haimfanyi apate hamu na wewe maana tayari ANAKUJUA

Ndo maana wanawake mnateseka kulilia wanaume huku mkiamini mnawahudumia kila kitu, Maana hamjui kwamba MWANAUME ANATAKIWA AJE KWAKO AKIWA NA PESA YAKE MWENYEWE haijalishi katoa wapi, Ndo maana wewe ukimpa AMANI anakwenda kutoa penzi zuri kwa Mwanamke mwenzio

Waswahili walipata kunena:-

Usidanganyike etiii kikubwa UPENDO WA DHATI
hayo mambo yanaweza kutajwa kwa MADARAJA kwamba Mwanaume asiye kuwa na PESA awe na Mwanamke ambaye atasubiri MUME aje na chochote, Ila sio Mwanamke una pesa umiliki Mwanaume asiekuwa nacho utegemee ATAKUPENDA hilo sahau, Kuna wakati uwezo wako utamkosesha AMANI na atakuwa mnyonge ila niamini IKO SIKU HALI YAKE HALISI IKIRUDI KI FIKRA hatakubari ujinga huo, Wanawake fikeni mahala MKUBARI KWAMBA MNAWAJIBIKA KUMTII MWANAUME itasaidia pia kujiepusha na KUWALEA WANAUME kwa kutaka wasiwe na sauti

