NI ATHARI ZIPI ZINAWAPATA WANA MAHUSIANO PAMOJA NA WANA NDOA WALIOPISHANA UMRI MKUBWA
Kwanza kabisa naomba nieleweke;-
UMRI HAUHUSIANI NA UPENDO MTU ANAWEZA KUPENDA AMA KUPENDWA NA MTU ANAYEMZIDI UMRI NA KUSIWE NA SHERIA KWENYE UHUSIANO AMA NDOA HUSIKA
Mapenzi yanabebwa na MOYO ndo maana waliobahatika kupata wenza wanaotumia MOYO kupenda muda wote huleta FURAHA NA AMANI kwa mwenza husika, Kama Mtu akikupenda kwa sababu muda wowote unaweza kupoteza hata FURAHA NA AMANI yako mwenyewe, kwani kila Bin adam anakuwa na uwezo wa kujitengenezea FURAHA NA AMANI inayotokana na ubinafsi wake, Hivyo anapokutana na Mtu asiye sahihi lazima ataambulia MAUMIVU yaliyotawaliwa na MAJUTO
Nirejee kwenye kichwa cha UJUMBE husika;
Mahusiano ama ndoa ambayo wawili hao kati yao mmoja ni mkubwa kuliko mwenzie lazima kuwe na limitation ya UMRI
Unaingia uhusiano au ndoa na mtu ambaye wewe ukizeeka atakuwa bado anahitaji STAREHE YA KITANDANI lazima uwe mhanga, Kwani wakati ambao Mmoja wao anakuwa amepoteza hamu ya MAPENZI mwenye umri mdogo atakuwa bado anahitaji, Mbaya zaidi mwenye umri mdogo atakuwa ANAJIONA BADO ANALIPA
Wakati huo vita ya MAPENZI itakuwa kwenye UAMINIFU na kwa vyovyote vile kama hakutakuwa na busara kati ya wawili hao lazima KUACHANA KUTAHUSIKA kwani upande wa mkubwa utalilia UAMINIFU na upande wa mdogo utalilia PENZI na kila upande kushindwa kuwa suruhu ya tatizo
Nini kifanyike kuepuka mahusiano au ndoa za aina hii;-
MTU KUJIPIMA MWENYEWE NA KUWEKA TAHADHARI YA KESHO YAKE ILI KUKWEPA MARADHI YANAYOTOKANA NA KUKATALIWA HUKU UKIWA UMEZEEKA