MWANAMKE ANAMILIKIWA KWA PESA ZAIDI KULIKO MAPENZI KWA SABABU PESA INAWEZA KUMJENGEA FURAHA NA AMANI BINAFSI
Kwanza fahamu kwamba maisha yanahitaji utimilifu wa mahitaji kuliko starehe kwa sababu starehe ni zao la ziada, Maana MAPENZI ni sehemu ya starehe na PESA ni kwa mahitaji stahiki, ndo Maana nasema:-


Mwanaume kama una akili unapashwa kujua wazi kila Mwanamke anahitaji kupata Mwanaume ambaye atamtimizia mahitaji yake yote ikiwemo TENDO LA NDOA japo nimejifunza kwamba:-

Usaliti unaosababishwa na NGONO ni wa kutafuta nafasi pamoja na maandalizi, Ila Mwanamke akiwa anahitaji PESA ili atimize mahitaji yake yupo tayari kusaliti kwa risk kwamba LIWALO NA LIWE hatajari hata atagundulika



Wanaume tafuteni pesa muone ilivyo rahisi kupata Mwanamke unayevutiwa nae pamoja na kuwa na hisia nae, Ila kama huna hela maana yake utalazimika kuingia kwa Mwanamke ambaye sio wa hisia zako wala hujawahi vutiwa nae upo pale kwa MTEREMKO

Nakwambia ukweli Mwanamke :-

Fahari ya MOYO wa Mwanaume ni pamoja na kuwa na Mwanamke anayempa matumizi, manao waona hawahongi mjue MFUKONI HAZIGAWANYIKI
