MWANAUME MJUE MWANAMKE UPATE KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA ZAKE

Awali ya yote Ifahamike kwamba MUUNGANIKO WA MWANAMKE NA MWANAUME NI MAPENZI

Kwa sababu UPENDO huinuliwa na SHAUKU na kwa vyovyote vile kinachounganisha hawa wawili ni MAPENZI kila upande kuhitaji upande wa pili, Ndo maana UPENDO unabakia kuwa zao la MAPENZI na ndo maana ya MIGOGORO MINGI YA MAHUSIANO PAMOJA NA NDOA NI UPANDE MMOJA KUSHINDWA KUKABILIANA NA MIHEMKO YA KI MWILI YA MWENZA HUSIKA.
Nirejee Kwenye Mada yangu:-

Mwanamke ni jinsia, Hivyo kama kuna tofauti ya Mwanamke ni ndogo sana ila kwa asilimia kubwa MWANAMKE ANABAKIA KUWA YULE YULE

Mungu amemjaalia Mwanamke kuwa na HITAJI KUU MOJA KWA MWANAUME nalo ni kutaka UPENDO 

Ndani ya hitaji hilo la Mwanamke kwa Mwanaume Kuna mlolongo mwingi wa MAHITAJI ikiwemo TIBA YA MWILI pamoja na MATUNZO 

Ndo maana nataka kusema:-


Ukiweza kumtunza Mwanamke anakuwa mzuri na atakuwa mwenye muonekano mzuri Sana kulingana na vile unapenda awe, vivyo hivyo kama Mwanaume atampa AMANI Mwanamke ni rahisi mno kwa Mwanamke kujiachia ki akili pamoja na ki mwili
ili ufaidi aina Tatu za radha yake.

Kama Mwanamke hana AMANI hawezi kuwa na UHURU wa MAPENZI na hapo ndipo utapambaana na ukavu pamoja na baridi, Ila kama ana AMANI huwa ni wa MOTO kwani mwili uko tayari



Hakuna UCHAWI Kwenye MAPENZI zaidi ya Mtu kuijua haja ya Mwenza wako, iwe Mwanaume hata Mwanamke ni ngoma drooo, Mwanamke ki maumbile ni MSIRI ndivyo zilivyo HISIA zake, na wenye heshima kwa Mwanamke ni wale waliojua HISIA ZA MWANAMKE ZIMEKAA UPANDE GANI



Mwisho kabisaaa :-

Kama ungelijua kwamba hakuna jipya Kwenye kubadili wanawake basi ungemfanya Mwanamke wako awe MPYA KILA SIKU
