TUKUMBUSHANE KIDOGO KUHUSU UAMINIFU!


Nguzo kubwa iliyoshikiria pendo baina ya mahusiano ni UAMINIFU "trust".

Maranyingi nguzo hii inapoyumba mahusiano yapo hatarini, hata penzi huelekea kufa.

Wakati mwingine uaminifu ni kama kioo, huwezi kukirudisha tena pindi kinapovunjika na unaweza kujiumiza mwenyewe kwa kujitahidi kuunga vipande vya kioo vilivyovunjika!

"Trust is just like a mirror, can't be fixed once it's broken, you'll end up hurting yourself"

Elewa kuwa samahani yaweza kurudisha penzi lakini kamwe haina uwezo wa kurudisha uaminifu uliopotea.

Once is gone is gone!

LINDA uaminifu ambao mtu anakuonyesha, tafadhali usifanye hiyana pale unapoaminiwa, yakupasa urejeshe thamani ya uaminifu unaopewa.

Mahusiano yako yatakuwa bora siku zote, penzi lako litanawiri, furaha na tabasamu litarejea usoni mwako, kazi yako itapendwa na hata watu wa karibu watajivunia uwepo wako.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA