BADO NATAFUTA -SEHEMU YA 08

BADO NATAFUTA
Mtunzi-Mniga Mputa
Sehemu. Ya. 08
WhatsApp:0678926045
Mniga alimkuta heppy anadeki sebleni pale akamsalimia,
'"Umeamkaje heppy mdogo wangu, alisalim mniga,
'"Salama tu kaka shikamo, alijibu salim heppy,
'"Marahaba sasa mimi ngoja nikachukuwe pesa yangu maana Jana sikuchukua, aliongea mniga,
'"Sawa kaka nakutakia kazi njema, aliongea heppy,
"'Asante mdogo wangu na wewe baki salama, aliongea mniga na kutoka zake huku njiani anawaza akipewa tu pesa cha kwanza ni kulipia kodi ya chumba ili ahame pale maana kachoka kunyanyasika, aliwaza sana mniga hadi alifika getoni kwa john ambae alimkuta ndo anamka,
'"Oya nambie mwana, aliongea mniga,
"'Poa kabisa mniga jamaa yangu, aliongea john,
'"Safi sasa vipi kuhusu pesa yetu maana Jana hatukuchukuwa, aliongea mniga,
'"Ni kweli nisubili basi nioge twende zetu tukachukuwe, aliongea john na kuingia bafuni kuoga kwanza mniga alibaki nnje huku katulia kimya hadi john akamaliza kuoga na akatoka alimkuta mniga pale pale,
"Aaah mniga jamaa mbona umesimama tu nnje wakati ndani kupo, aliongea john,
'"Hapana nikajuwa labda kunashemeji maana na wewe hujambo, aliongea mniga kwa utani na kucheka sana,
'"Duuh Jana nilichoka sana hata sikuwa na hamu nae yani, aliongea john na wakaingia ndani wote,
'" ila mniga rafiki yangu ujuwe unanipa mashaka sana ujuwe, aliongea john baada ya kufika ndani na kukaaa kitandani,
'''Mashaka gani tena john rafiki yangu, aliuliza mniga,
'"Unajuwa tangia utoto tumecheza wote hadi sasa ukubwani sijawahi kukuona umesimama na mwanamke au unadem pembeni, aliongea john kwa utulivu zaidi, mniga alinyamaza kimya kidogo badae akamjibu john,
'"Nikweli john ila unajuwa Mimi kwa sasa nafikilia maisha kwanza mwanamke badae nikishapata ndo ntatafuta, aliongea mniga kwa ulfu kidogo,
'"Hahahaha unanichekesha kweli jamaa yangu sema tu kama jogoo hapandi mtungi nikutafutie dawa jamaa yangu, aliongea john na kucheka,
'"Utani sasa john rafiki yangu nani kakwambia kwamba hapandi mtungi, aliongea mniga,
'"Sijaambiwa na mtu ila najionea mwenyewe ila tuachane na hayo basi twende kwanza kwenye pesa, aliongea john,
'"Kweli kabisa umeongea LA maana, aliongea mniga na wote walitoka huku wanapiga story nyingine mdogo mdogo hadi walifika kwenye godaoni LA Jana walipoingiza mahindi kama bahati kwao walimkuta bosi nae ndo anataka kuondoka,
'"Oh vijana mngechelewa kidogo tu Mimi ningeondoka zangu, aliongea bosi yule,
'"Duuh kumbe tungepishana na msimu jamani, aliongea john na kumsogolea bosi,
'"Shikamo mzee wangu, aliongea john
'"Marahaba naona Jana mlijitahidi sana hadi mkamaliza kuingiza mahindi yote, aliongea mzee yule,
'"Ndio mzee niliona kama tukiacha kumaliza Leo tungesikia uvivu sana, aliongea john
'"Sawa hakunashida chukuwa pesa yako, aliongea mzee yule na kumkabizi john pesa zao,
'"Asante sana mzee wangu acha sisi tuondoke zetu, aliongea john,
'"Sawa ila kesho kama hamtajari ntakupigia simu ili mje kupakia sembe kwenye gari, aliongea mzee,
'"Hakunashida mzee wangu wewe ukiwa na kazi yoyote niambe tu, aliongea john,
'"Basi sawa kijana, aliongea mzee na kupanda gari john akamsogelea mniga
"'Sasa kila mmoja afe na chake mniga, aliongea john, na kuanza kuhesabu pesa ambapo ilikuwa ni laki tatu keshi akampa mniga laki na hamsini huku na yeye akabaki na laki na hamsini,
'"Sasa John nipeleke kwenye nyumba hiyo Mimi nikalipie kabisa, aliongea mniga
'"Duuh kumbe jamaa yangu unaakili sana wewe twende zetu, aliongea john na safari ikaanza huku kila mmoja anafuraha sana ya kupata pesa hatimae walifika na john ndo alikuwa mwenyeji alibisha hodi na wakasubili kidogo alitoka mmama wa makamo,
'"Oh john kijana wangu umekuja tena, aliongea mmama yule,
'"Ndio mama shikamoo, aliongea john na mniga nae akasalimia,
'"Marahaba wanangu nawasikiliza sasa nyie, aliongea mmama yule,
'"Ndo nimemleta mwenzangu ambae anataka chumba ndo huyu, aliongea john,
'"Oh sasa kijana chumba umepata ila kwa mwezi ni 30,000 tu kama unalizika sawa kama utashindwa sawa, aliongea mmama yule,
'"Kaniambia john na nikalizika mama ndomaana nimekuja hapa, aliongea mniga,
'"Oh basi sawa nipe pesa nikupe funguo yako, aliongea mmama yule mniga akatoa laki na hamsini akamkabizi mama yule ambae alipokea na kuhesabu akamjibu,
'"Sasa mwanangu umelipia ya miezi 5 utakaa hapa bila buguza yoyote, aliongea mmama yule,

Kwa 1500 tu unajipatia story hii mbaka mwisho lipia kupitia Tigo Pesa 0678926045 au Halo Pesa 0620816989 ukilipia  ntumie ujumbe wa muamala wako WhatsApp au Facebook Inbox)

Itaendelea.................

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA