BADO NATAFUTA SEHEMU YA 11

Mtunzi-Mniga Mputa
Sehemu. Ya. 11
WhatsApp:0678926045
Sasa john ukitaka kunijuwa mimi kuwa Mimi jogoo hapandi mtungi basi nipe Dada yako yule angel ndani ya mwezi mmoja tu kama hajapata ujauzito hapo ndo utajuwa mimi mgonjwa kweli, aliongea mniga huku yupo kauzu kweli,
'"Aah jamaa yangu mniga sasa huo utani wa kijinga Dada tena, alioƱgea john kwa kupayuka,
'"Oh kumbe imekuuma basi ndo ujuwe kuwa na mimi nimeumia sana ulivoniambia kuwa jogoo hapandi mtungi, aliongea mniga huku anacheka,
'"Basi poa yaishe mshikaji wangu vipi naona ulikuwa unamtazama mtoto wa mama mwenye nyumba, aliongea john kwa kuuliza,
'"Daaah nilikuwa nasaficha kidogo macho bhana maana unanisema sana, aliongea mniga kwa kutabasamu,
'"Duuh kweli kazi ipo maana huwaga watu kama nyinyi mnakuwa hamu sana tofauti na kama mimi hivi, aliongea john
'"Hahahaha sawa bhana nisubili nichukuwe vitu ndani ili nije kupika hapa hapa nnje tukipiga story bhana, aliongea mniga na kuingia ndani alichukuwa vitu vya kupika na sufuria huku akitoka navo nnje na kukaa mlangoni kwake akianza kupika huku john apiga story,
'"Oi mniga muangalie mtoto yule jinsi alivo kama hakanyagi chini jamaa, aliongea john na kumfanya mniga ageuke kuangalia,
'"Duuh kweli mzuri ila anakanyaga chini bhana achaga mbwe mbwe zako, aliongea mniga huku anacheka kidogo,
'"Kweli mniga jamaa maana ndo ule msemo usemao wenye pesa wanafaidi sana ni kweli, aliongea john
'"Ndo maana nimekwambia john tutafute pesa kwanza wanamke badae ndo utafaidi sio sasa na pesa huna siutakula kwa macho tu, aliongea mniga sauti ya chini kidogo maana yule mrembo alikalibia kufikia pale,
'"Nikweli tutafute ila mimi mniga siwezi kuishi bila kuduu na mwanamke bhana, aliongea john,
'"Sasa ndo utakoma ona mimi sijawahi kuduu na ndomaana sipati shida kama wewe naona kawaida tu yani, aliongea mniga huku anamcheka john huyu yule mrembo aliwafikia na kuwaambia,
'"Samahani kaka zangu aliopangisha kwenye chumba hicho mmoja au wote mnakaa, aliongea yule mrembo kwa sauti yake tamu,
'"Anakaa mmoja tu ambae huyu mimi nimekuja tu kumtembelea, alijibu john haraka haraka na kufanya mniga nusu acheke,
'"Oh kumbe sasa wewe kaka yangu hapa umepanga mwenyewe sasa kuwa makini maana sisi kwenye nyumba yetu hatutaki mtu ambae anabadilisha wasichana kama nguo kama unamchumba basi ajage huyo huyo, aliongea mrembo yule,
'"Sawa Dada yangu usihofu kwa maana mimi hata huyo mchumba sina na sinaga habari na wasichana mimi, aliongea mniga,
'"Basi itakuwa vizuri na usijiulize kwani kama nakupangia hapani ila tuliwahi kumpangisha kijana mmoja hapa na ilikuwa balaa maana yeye kila kukicha anabadilisha tu sasa sikumoja aligonganisha hapa wasichana na ikawa balaa maana walipigana nusu wauane ndomaana nikakupa latiba hiyo samahani lakini, aliongea yule mrembo kwa kumaliza kuhadithia,
'"Usiwaze Dada yangu mimi sinaga tabia hiyo bhana, aliongea mniga,
'"Sawa kwahelini mimi naenda zangu kesho tena ntakuja, aliongea yule mrembo,
'"Sawa ila tufahamiane bhana hata majina, aliongea john kwa haraka sana,
'"Oh nikweli mimi naitwa jeni sijajuwa wenzangu, aliongea mrembo yule,
'"Na mimi naitwa john huyu mpangaji wako anaitwa mniga, aliongea john,
'"Nashukuru kuwafahamu, aliongea jeni,
'"Hakunashida Dada ila tu ukiwa na kazi usisite kutuambia maana ndo maisha yetu yakuunga unga, aliongea john,
'"Msijari ila labda elimu yenu mngeniambia maana ntaweza kuwaunganisha kwenye kampuni ya baba yangu, aliongea jeni,
'"Kwa mimi nimesoma hadi kidato cha nne ila huyu mniga aliishia LA saba tu, aliongea john,
'"Duuh kwa wewe kidogo utaweza kupata kazi ila huyu wa darasa la saba ndo haitawezekana kupata, aliongea jeni kwa sauti ya upole kweli,
'"Kwangu mimi hakunashida bhana kama akipata john basi safi tu wala msiniwazie sana, aliongea mniga huku akiendelea kupika zake,
'"Mmh mbona kuma umejitenga jamani, aliongea jeni
'"Hapana maana john ni rafiki yangu wa utotoni hadi sasa akipata sawa sawa na mimi nimepata tu ananipa tu vimiatano tano huku na mimi nakomaa, aliongea mniga kwa upole
'"Sawa basi wewe john kesho nikija nikukute hapa kwa mniga na vyeti vyako, aliongea jeni na kuanza kuondoka,
'"Sawa Dada jeni hakunashida, aliongea john kwa furaha sana,
'"Ukipata kazi inatakiwa ufanye kwa bidii na vimke vyako uviache maana vitakuhalibia maisha yako, aliongea mniga kwa kumshauli rafiki yake kipenzi,
'"Usijari ntapambana na nikilipwa mshahara wa kwanza tu lazima ntakupa msingi wewe ufanyage biashara, aliongea john huku wote wakacheka,
'"Duuuh kweli kazi tunaanza kupanga kabla hata kazi hujapata bhana, aliongea mniga na kuzidi kucheka,

Kwa 1500 tu unajipatia story hii mbaka mwisho lipia kupitia Tigo Pesa 0678926045 au Halo Pesa 0620816989 ukilipia ntumie ujumbe wa muamala wako WhatsApp au Facebook Inbox)

Itaendelea..............

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA