UNAPOMSAIDIA MWANAUME JUA HUJAMNUNUA SI LAZIMA AKUOE!


Wanawakwe wengi wanaopenda sana wakidanganywa kidogo kujisahau katika kutengeneza maisha yao na kutengeneza ya wanaume wao. Unakuta binti yuko bize kuhangika kijana kupata kazi kwakua tu anampenda na anaamini ndiyo atakua mume wake lakini wakati huo labda yeye hana kazi au ana kazi lakini haiingizi kipato cha kihivyo.

Niwape tu ujumbe dada zangu kuwa, unapomsaidia mwanaume kufanikiwa haimaanishi kuwa umemnunua. Mwanaume sio kochi kwamba ukilinunua ni lazima ulikalie hapana. Mwanaume ni kiumbe hai na ana hisia. Unapomsaidia kufanikiwa akishafanikiwa anamaamuzi ya kukuoa wewe au kuoa mtu mwingine. Kamwe usidhani kuwa eti kwakua ulimpa mtaji au ulitafutia kazi ndiyo lazima awe mume wako.

Hapana, hummiwili huyo mwanaume, unaweza kumsaidia kufanikiwa halafu akachoka kukupenda. Kumsaidia halafu akagundua kuwa kumbe wewe si wa hadhi yake alikua anakupenda kwakua alikua masikini sasa hivi amepata pesa hamuendani. Dada najua utasema unamuchia Mungu lakini hembu nitajie Kitabu gani cha Mungu au hata cha shetani ambacho kimesema umpe mwanaume mtaji afanikiwa ili akuoe? Unapotoa toa kwa moto lakini ushdani kama umemnunua mwanaume!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA