SIRI NYINGINE YA KUMPATA MUME/MKE SAHIHI NA KUJUA MAPEMA KAMA NDIYE.


Sote tunajua Mungu ndio anayeozesha watoto wake wanapofikia wakati wa kuoa na kuolewa.
Wazazi wa kimwili huwa wanakamilisha tuu alichokiunganisha Mungu.
Baada tu ya kuokoka kabla ya kukimbilia kuoa au kuolewa; lilia sana kulijua kusudi la kuwepo kwakwo hapa Duniani, yaani Mungu kakuleta hapa duniani ili ufanye nini katika kuujenga Ufalme wa Mbinguni.
Hata Mungu atakapomleta binti/kijana kwa ajili yako haitakusumbua sana kujua kuwa ndiye, kwa sababu kama kweli ni Mungu ndiye kamleta hatakuwa mtu ambaye yupo nje ya kusupport huduma ambayo Mungu kaiweka ndani yako...........lazima mtaendana tu kihuduma kama ndio yeye.
Kuoa au kuolewa kabla haujaifahamu huduma ambayo Mungu kakupatia kwa ajili ya kutumika kwayo, ni sawa na mtu anayecheza kamari, “kuna kupata na kukosa.”
Kitu ambacho sio sawa kwa watoto wa Mungu.
Mike Jr
May be a close-up of 1 person and people kissing

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA