UNAUMIZWA NA MAPENZI? JIBU HILI HAPA!


Kwenye ulimwengu wa wapendanao, wengi sana wanaumizwa. Wanateseka. Wanaambulia maumivu katika kila uhusiano wanaouingia kutokana na sababu mbalimbali.
Wengi hujikuta wakilia kwa kuingia kwenye uhusiano na watu wasio sahihi. Kuna wengine wanajikuta kwenye maumivu kwa sababu ya tabia zao wenyewe. Uhusiano madhubuti, unajengwa na chaguo sahihi. Ni mtu gani ni sahihi kwako? Anayepaswa kuwa mwenzi wako anatakiwa kuwa na sifa gani?
ANZA KUJITATHIMINI
Ili uweze kujua unapaswa kusimamia wapi katika mahusiano, unapaswa kujitathimini kwanza wewe mwenyewe. Ujue ni aina gani ya uhusiano unaoutaka. Kuna ule uhusiano wa kuwapoteza muda ili tu usiwe mpweke na kuna ule uhusino wa malengo.
Wapo watu ambao hawahitaji kuwa na uhusiano endelevu. Macho yao yanaangalia walipo, mengine ni majaaliwa. Hawana muda wa kufikiri kwamba kuna maandalizi yanapaswa kufanyika hadi kufikia kwenye kilele cha mafanikio, ndoa.
Wao wanafurahia ujana. Mwanamke anataka ‘boyfriend’ ambaye atajiachia naye klabu, atakayemudu gharama mbalimbali kama vocha, saluni, kiatu kizuri au gauni kali. Kundi hili ndilo lile la wale wanaofurahia maisha ya kujirusha na pesa kwa sana. mwanaume ukiwa huna pesa au pengine gari, hakuelewi. Wenzake atawaringishia nini kama wewe huna gari? Wenzake watamuonaje?
Yeye starehe kwanza, mengine hayana maana. Kwenda kujionesha kwa wenzake katika kumbi za sinema ni jambo muhimu na kumfanya aonekane anaenda na wakati kuliko kitu kingine.
Mwanaume wake akipoteza sifa hizo, anamhama. Anazima na kuwasha penzi kama vile swichi ya kuwashia taa. Jioni ana huyu, asubuhi ana mwingine na anamsahau kabisa yule wa jioni kwa kipindi kisichopungua saa 24.
Kundi la pili ni la wale wanaotazama mbali. Macho yao yanavuta taswira ya mbali ya kufika kwenye kilele cha mafanikio ya ndoa. Kundi hili ndilo linalokumbww na madhara makubwa kwa sababu linawekeza ‘safari’ yao katika imani zaidi. Hapa ndipo wengi wanapopata maumivu kwa sababu, penzi ndilo linalozalisha maumivu kwa yule ambaye anaingia kwenye uhusiano na mtu ambaye si sahihi.
Nadhani, kila mmoja anatambua kwamba ukimpenda mtu huwa anamuweka moyoni. Moyo ukishapenda, ni vigumu kuubadili. Moyo una kawaida ya kuganda kama ruba. Ukipenda ndio umependa.
MTATHIMINI UNAYETAKA KUWA NAYE
Usikurupuke kuingia kwenye uhusiano. Ukishajitathimini na kugundua kwamba unahitaji mwenza wa maisha, anza kujua sifa zake. Usikurupuke kuuzamisha moyo wako kwa mtu kabla hujajiridhisha kwamba ni mtu sahihi. Mchukulie mwenzi wako kama rafiki, msome tabia na ukiona ana sifa zile unazohitaji, zile za malengo ya mbali, unaweza kuruhusu uhusiano uanze sasa.
Utampenda zaidi endapo utakuwa umeshajiridhisha kwamba uliyenaye, ana sifa za kwenda safari ndefu au fupi. Kama ni ndefu, mweke karibu na uanze kupima utu wake. Mtathimini kama naye ana upendo wa dhati kwako. Havutwi na tamaa? Si mtu wa kuendekeza starehe? Ni mvumilivu, anakujali? Anaguswa na matatizo yako? Mtu hawezi kuficha tabia mbaya kama mtakaa katika kipindi cha miezi mitano, sita hadi mwaka.
Ukiona mmepita kipindi hicho huku moyo wako ukiridhika na upendo anaokupa, kukujali na kukuthamini basi ni wakati wako sasa kuwekeza mara dufu upendo wako kwake. Muombeni Mungu na muanze kuzungumzia mipango ya ndoa. Kwa msaada wake, mtafanikiwa safari yenu. Muanze na Mungu kuanzia hatua ya kwanza hata kuendelea.
Tukutane wakati mwingine kwa mada nyingine nzuri. Tunaweza kuwasiliana DM kwa maswali, ushauri au kubadilishana mawazo pia.
Luckson Massatu
May be an image of 1 person, standing and indoor
58
3 shares
Like
Comment
Share

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA