HAKUNA MWANAUME MENYE AKILI TIMAMU ATAOA MWANAMKE WA AINA HII!

 

“Ni ngumu sana kwa wewe kupata mwanaume mwenye akili wa kukuoa.” Nilimuambia baada ya kuongea naye kwa zaidi ya nusu saa.
“Kwanini Kaka, imnamaana mimi si mzuri?” Alijibu huku akitaka kulia, nilimuona kabisa amekata tamaa ya maisha kama vile amechoka kuwa mwenyewe.”
“Hapana, ni kwakua unatembea na mume wa mtu hivyo kila mtu anakuona kama mdangaji, wanaume wenye akili wakija kukuulizia wanaambiwa unatembea na mume wa mtu, unamdanga, ndiyo amekupangishia nyumba na ndiyo kila kitu kwako. Wanakuona kama unapenda pesa, ila wanaume wadangaji wakija wakisikia unatembea na mume wa mtu wanajua wewe ndiyo mzuri, wanakutongoza wanapita na wewe kisha wanakuacha ukidanga.”
“Kaka usiseme hivyo, mimi sitembei na mume wa mtu, huyu Kaka ni rafiki yangu tumezoeana naye hata mke wake ananijua, ananichukulia kama rafiki yake tu!” Ananiambia, mimi nacheka kisha namuambia.
“Dada, kutembea na mume wa mtu si lazima kufanya naye mapenzi, ile kuonekana tu unazunguka naye ni kutembea naye. Mume wa mtu anakuja kwako, unampikia, anakaa mpaka saa nne usiku anaondoka.
Mume wa mtu kila siku mko naye, haendi kula Kitimoto na mke wake lakini kutwa kucha umemganda unaenda naye. Kila mkitoka kazini anakuleta nyumbani, ukiwa na shida yoyote unamuambia, nakuja akikiambia kukusaidia. Kwenye Part za ofisini kwake unaenda wewe eti mnajiambia mke wake si mtu wa kutoka, kwenye Biashara zake unasimamia wewe eti unajifanya kuwa wewe ni mtu wa Biashara.
Dada hakuna, narudia hakuna, narudia hakuna mwanamke mwenye akili timamu ambaye anafurahia mume wake kuwa na rafiki kama wewe, narudia hakuna, tena anahisi unatembe naye na alishajaribu mara kibao kumuambia mume wako aachane na wewe ila mwanaume labda kwakua anaona hafanyi mapenzi na wewe anajiona kama hachepuki.
Dada huyo mwanaume anamuumiza mke wake kuliko kufanya mapenzi na wewe. Hii ni kwakua wewe si kama mchepuko bali kama mke wake, kama Dada yake na kama rafiki. Kwamba mwanaume anakupa umuhimu wewe kuliko, dada, rafiki na mke. Kwa kifupi ni kwamba unatembea na huyo mwanaume na kama hutaacha kuzunguka na mume wa mtu kila siku basi jua ndoa utaishia kuziona kwenye mitandao!
Dada acha kumsumbua Mungu kila siku unahangaika kwenye maombi kuomba mume wakati mume unaye kutwa kucha kuzunguka na mume wa mtu! Narudia haijalishi kama unatembea naye au la lakini kama kila siku watu wanakuona unazunguka naye basi unatembea naye, unamkera mke wake, hembu vuta picha umeolewa halafu mume wako ana rafiki kama wewe utafirahi?”
MREJESHO; Maneno yako yaliniingia sana Kaka, nilikaa na kufikiria nikaona kabisa kuwa nakosea, kila mtu alikua anajua ni mpenzi wangu. Hata nilipowauliza rafiki zangu kumbe nao walikua wanajua kuwa natembea naye. Kaka hapa mtaani kila mtu alikua anajua kuwa ni mwanaume wangu. Nilichofanya ni kupunguza mawasiliano na huyo Kaka.
Mwanzo alikua hataki ila nikamuambia akahangaika na ndoa yake na mimi natafuta yangu, niliihama kabisa ule mtaa, nilikua naishi zangu Kimara nikahamia Kindondoke, hakuna anayenijua ni mtu mpya kabisa. Alikua nakuja kuja kazini kwangu nikamuambia mazoea, yaani nina mwaka sasa sijawahi kuonana naye wala kuwasiliana naye.
Kaka nashukuru uliniambia ukweli, nimeingia kwenye mahusiano mwaka huu na naona yanaenda vizuri, sitaki tena mazoeazoea na wanaume ambao wanavuka mipaka. Nadhani Kaka upweke ndiyo uliokua unanifanya nihangaike naye, sasa hivi nimejua alivyokua anajisikia mwanamke mwenzangu kwani mpenzi wangu naye kulikua na kadada kanataka kunizoea nikakakacha kwani sitaki shobo tena.
MWISHO
May be an image of 1 person and standing

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA