KITU KIMOJA AMBACHO KILA MWANAMKE ANATAKIWA KUKIJUA KAMA ANATAKA MWANAUME AMUAMINI!


Una ndoa ya mwaka mmoja lakini ushaanza kulalamika kuwa mume wako anwapenda zazidi ndugu zake, hakupendi anapenda zaidi marafiki zake, hakushirikishi kwenye mambo yake anashirikisha zaidi ndugu na marafiki zake.
Ngoja nikusanue Dada yangu, ili mwanaume kuanza kukushirikisha kwenye mambo yake ni lazima kwanza akuamini, kama hakuamini basi hatakushirikisha kwenye mambo yake na utaona kama anawashirikkisha zaidi ndugu zake.
Ukweli nikuwa, si kama anawapenda zaidi ndugu zake bali anawaamimi zaidi ndugu zake kwakua amewajua muda mrefu hivyo anajisikia vizuri sana kuwashirikisha mambo yake kuliko wewe ambaye ndiyo kwanza mmeanza kuwa marafiki.
Sasa unapoingia kwenye ndoa, moja kwa moja ukaanza kumuulizia kuhusu mali zake, ana kwianja unaanza kuulizia kina majina ya nani, ana Biashara nafanya na Kaka yake unaanza kumuambia amuondoe Kaka yake, kila kitu anamuambia Mama yake unaanza kumuuliza kwanini moja kwa moja unamfanya aikuamini.
Unamfanya anaanza kuwaza “Hivi huyu ni mke au kaja kwaajili ya mali zangu, mbona anaulizia sana kuhusu mali zangu kuliko ndoa? Mbona anachukia sana ndugu zangu?”
Ushauri wangu, najua ulitegemea ukishaolewa wewe ndiyo uwe kila kitu chake, lakini ukweli nikuwa, ndoa haikufanyi kuwa kila kitu chake bali matendo yako ndiyo hukufanya kuwa kila kitu chake, acha kuulizia kuhusu mali zake, ndugu zake, kulalamika kama hakushirikishi, jipe muda wa kumsoma, muonyeshe uaminifu wako, shauri namna ya kufanikiwa atakuamini na utakua kila kitu chake!
May be a close-up of 1 person and glasses

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA