MAMBO 5 YA KUYAJUA KATIKA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII CHUNGA USIUMIZWE!

(1) Mwanaume anayekutongoza kamwe usimchukulie kama ni mpenzi wako mpaka pale mtakapoonana, ukajua anaishi wapi na anapofanya kazi kisha mkawa kwenye mahusiano ya uso kwa uso sio hayo ya kwenye mitandao, kuna watu wana watu wao na kuna wake zao huku wanalalamika kuwa mijamaa inakesha kwenye mitandao kuwa makini.
(2) Kama umeolewa au upo kwenye mahusiano siriasi acha kushobokea wanaume kwenye mitanado, acha kula pesa ya mwanaume kwenye mitandao kwa kisingizio kuwa hawezi kuniona, mtu umeweka picha zako kwenye mitandao na namba ya simu umempa ili akutumie pesa halafu unaanza mambo ya kusema hatujuiani akitaka kukujua anakujua na siku mume au mpenzi wako akiona hizo shobo anakuacha.
(3) Ogopa mwanaume anayemba pesa katika mitandao baada ya kukuahidi ndoa kisha Mama yake anaume au anapata matyizo, lakini ogopa zaidi mwanaume anayetoa hela kiholelaholela, yaani ukimuomba tu hata hamjawahi kuonana anakutumia pesa kuliko hata mpenzi wako ambaye unaenda kupika na kufua zile nguo, aisee hawa watoaji pesa kuna siku atakupiga tukio hutaamini, si wote ni matapeli ila wengi ndiyo michezo yao.
(4) Kwanza cha kumtumia picha mtu ambaye humjui, lakini kabla ya kutuma picha yoyote kwa mwanaume jiulize hivi hii picha naweza kumtumia Baba yangu mzazi, kama huwezi kumtumia Baba yako mzazi hiyo picha sio tu usitume bali usipige. Achana na ujinga wa kusema natuma nusu tu, natuma maziwa tu, natuma sijui nini, kwanza ni kujidhalilisha pili kama uko kwenye mahusiano picha nusu inakuharibia kwakua hiyo nusu uliyoituma mtu wako anaijua.
(5) Hapa hakuna hata namba tano, ila nilitaka tu kukuambia kuwa nina vitabu vinne, cha kwanza ni “Ndoa Yangu Furaha Yangu, Biashara 50, MWANAUME na Interview na ajira. Bei ya Kitabu kimoja ni shilingi elfu kumi tu. Unalipia kwa M-Pesa No. 0742-381-155 au Tigo Pesa No. 0657-552-222 na hakikisha jina linakuja IDDI MAKENGO.
May be an image of 1 person and footwear

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA