TAZAMA NYUMA KWA KUJIFUNZA SI KWA KUJUTA


Kila kitu kilichotokea katika maisha yako hakikutokea kwa bahati mbaya, kuna sababu ya kila kitu kutokea hata kama ni kibaya.
Chukulia changamoto ulizopitia katika maisha yako kama darasa na kamwe usiangalie nyuma kwa kusononeka na kujilaumu. Acha kuumiza kichwa katika mambo ambayo sasa huwezi kuyabadilisha.
Kumbuka ubaya wa jana nikuwa imeshapita, haiko tena mikononi mwako na huwezi kuibadilisha, lakini kesho bado haijafika na unaweza kuitumia leo kutengeneza kesho yako nzuri kwa kujifunza kutoka jana.
Kuna mambo mengi ambayo yamepita ambayo kama ungepata nafasi ungeyafanya tofauti. Yachukulia mambo hayo kama darasa na anza kufanya tofauti sasa. Wewe kuwa hai leo ni nafasi ya kuyabadilisha mambo hayo na si kuendelea tu kujuta.
Image result for happy black coupleAcha kuishughulisha akili yako katika kujuta, acha kupoteza muda wako katika majuto katika kuwaza laiti ningelifanya hivi aua vile, fanya sasa ambavyo ungetamani kufanya.
Kuna namna ambavyo uliumizwa awali au namna ambavyo ulimuumiza mtu na sasa unajuta. Hembu jisamehe kwa kuumiza mtu na msamehe aliyekuumiza kisha endelea na maisha. Kumbuka hatuishi kurudi nyuma bali kwenda mbele.
Jifunze na endelea na maisha ukiwa unajua ulikosea wapi ili usiyarudie tena yale makosa. Usijute na kujionea huruma kwani ukishaanza kujionea huruma ni ngumu sana kwako kuendelea mbele.
May be an image of 1 person and standing
Steve Martine and 1.7K others
193 comments
106 shares
Like
Comment
Share

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA