NIHERI KUBAKI NA MALAYA WAKO KULIKO KUONDOKA KWENDA KUWA MCHEPUKO!


Wakati sasahihi wa kuacha kumfuatilia Mwanaume wako ni pale unapofunga naye ndoa au kuamua kuishi naye na kutengeneza familia. Kwa uzoefu wangu nimegundua mambo haya;
(1) Hakuna mwanaume anayebadilika kwa kufuatiliwa bali wanaume wengi huzichoka ndoa zao kwa kufuatiliwa. Kumfumania na kuanza kumpa shule ya madhara ya kuchepuka ni kama kichocheo cha kuchepuka.
(2) Wanawake wengi wanaochepuka na waume za watu wanajua hivyo alishajiandaa na simu yako, mesjei zako na matusi utajisumbua bure humtishi na hakuna cha laana yoyote ambayo utamuachia itamfanya kuogopa kutembea na mwanaume wako.
(3) Ukimfumania mwanaume zaidi ya mara mbilia nazoea hivyo michepuko yake inaacha kuwa michepuko na kuwa wake wenza wako hivyo ukishamfumania mara moja acha kabisa kumfuatilia la sivyo utaishia kuchanganyikiwa na visirani vyako.
(4) Kusema kuna magonjwa mengi wakati hata ukijua bado unaendelea kufanya mapenzi naye hakusaidii chochote hivyo ni bora kuacha kuchunguza na kumuachia Mungu kuliko kuchunguza na kubaki na wasiwasi.
(5) Wanawake wengi wanaotoka kwenye ndoa kwakua wanaume zao wanachepuka mwisho wanaishia kuwa michepuko. Wengi wanasema namucha huyu mwanaume sitaki mwanaume mwingine tena, lakini baada ya mwaka upweke unazidi, hamu inazidi wanajikuta wanatamani kuwa na mtu, vijana wanwakimbia au ni wasumbufu hivyo mwisho wa siku wanatafuta watu wazima, wanaishi kuwa michepuko nao kupigiwa ismu kutukana.
(6) Umekubali kuingia kwenye ndoa kama hakudundi achana na simu yake, acha kumfuatilia kwani wakati mwingine anaweza hata asiwe anachepuka ila kwa kuchunguza ukahisi anachepuka ukabaki na kisirani chako. Niheri kubaki na malaya wako kuliko kuondoka kisha unageuka kuwa mchepuko.
May be an image of 2 people

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA