KAMA MWANAUME HUMTAKI UNAMBLOCK, NARUDIA UNAMBLOCK NA SI KUMUAMBIA SIKUTAKI!


Kama Mwanaume humtaki basi unamblock na akitumia namba nyingine nayo unaiblock na nyingine nayo unaiblock, meseji zake hujibu bali unazifuta. Lakini kama Mwanaume anakutafuta kila siku unaongea naye unamuambia kuwa humtaki hujamblock huyo Mwanaume anajua kuwa bado unamtaka hivyo ni sitaki nataka.
Tena kama uko kwenye mahusiano na Mwanaume wako, kusema nina mtu halafu unapokea simu zake ni kama vile umemkubali, narudia kama una Mwanaume ambaye unampenda na upo kwenye mahusiano au ndoa lakini kuna lijamaa kunakusumbua basi liblock.
Narudia, hata kama anatumia namba mia ziblock zote, lakini kusema nimemkataa ila hujamblock mwanaume hatakuelewa. Narudia, mblock, mblock, sijui kama mmenielewa Dada, najua unasema nishamuambia kuwa simtaki, lakini ipo siku atatuma meseji uya hovyo na wanaume hatusamehi kirahisi, najua mblock!
NB; Subiri ukishaachwa ndiyo utasema nilishamuambia simtaki, au ndiyo ulalamike inamaana ananiacha kwa sbabau hii?
May be an image of 1 person

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA