UNAWEZA DHANI MUME KAKUTELEKEZA KUMBE WEWE NDIYO UMEJITELEKEZA!


Dada zangu mlioko kwenye ndoa na mahusiano, ni lazima muwe na vipaumbele kwenye maisha yenu. Narudia, kabla ya kumlalamikia mume wako ni lazima kujiuliza hivi hiki kitu ninachokilalamikia kinafaida kwangu au kitanizidishia mawazo na migogoro tu! Labda niwape mifano midogo;
(1) Kila siku unalalamika kwa mashoga zako au kumnunua mwanaume kuwa hakujali kwakua tu hajakupost Instagram, hajakumbuka siku yako ya kuzaliwa, lakini mwanaume huyo anakuhudumia chakula, mavazi, kakupa na mtaji na mnajenga!
(2) Mwanaume unaishi naye, hujawahi kumfumania lakini unalalamika kuwa akiwa kazini hakukumbuki, sasa mtu hujawahi kumfumania, anahudumia familia, anakujali ameacha hela ya chakula nyumbani lakini bado mchana unataka akutumie meseji kukuuliza kama umekula au la?
(3) Anaacha matumizi nyumbani, unaweza kujibana hata ukamtumia Mama yako, ukajibana hata ukanunua kakiwanja kako, ukajibana hata ukafungua kabisshara, ukajibana ukanunua nguo za watoto, lakini bado unalalamika kuwa tangu uolewe mwanaume wako hajakupa pesa ya kununulia hata chupi au kuwapa ndugu zako.
Hivi unadhani huyo mwanaume ni mjinga hajui kuwa akiacha elfu kumi inatosha kwa kula ila anacha elfu ishirini ili kama mke ujiongeze au unataka kuelekezwwa leo fanya hiki fanya kile!
(4) Punguza kisirani dada yangu, ndoa ni tamu lakini ukishaanza kuiwekea malimau haiwezi kuwa tamu. Kabla ya kulalamika jiulize hivi hiki kitu natakiwa kukilalamikia kweli au kina maana kweli, sijui kama mnanielewa dada zangu!
May be an image of 1 person

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA