MWANAUME HATA KAMA MKE WAKO NI SHETANI ONDOKA KULIKO KUMPIGA
Wanawake si malaika, ipo siku atakukosea, lakini vyovyote vile hembu jaribu kujizuia kumpiga mwanamke. Wakati mwingine hembu amua kuondoka kuliko kumpiga au amua hata kukaa kimya, wakati mwingine hata mpuuze, si kama unamnunia hapana, mpuuze, wakati mwingine badilisha kitu. Labda ulizoea kumpa hela ya matumizi anza kununua vitu mwenyewe na muambie sababu ni nini? Siwaambii hivyo kwakua nawatetea wanawake, hapana, nawaambia hivyo kwakua unapoanza kumpiga mwanamke unatengeneza mazoea ya kumpiga.
Kuna wanawake ni mashetani, narudia kuna wanawake ni mashetani kuliko shetani mwenyewe, anakufanyia mambo mpaka unajiona kama si mwanaume, anakutesa kiasi kwamba hata ukitoka nje unakua huna amani, unajiona kama mjinga, unahisi kuchanganyikiwa, unakua kama chizi, narudia kuna wanawake mashetani. Lakini kumbuka, kama wewe si mshenzi ukishafungua ukurasa wa kumpiga mwanamke basi jua ushaharibu maisha yako. Hutakuja kuwa na amani, wakati mwingine hata ukija kukutana na mwanamke mwenye akili, ambaye mnataka kutengeneza maisha unakua ni mtu wa hasira, mtu wa kupiga na maisha yako yanasimama.