Mwanaume na mwanamke mnisikilize kwa makini mwenza wako anakiu ya kupata mwenza mwenye kukidhi haja na kukata kiu yake na sio kuoa jinsia yake.
Ana kiu ya kuishi na partner, rafiki wa maisha atakayempeleka kwenye mafanikio ya kiuchumi,afya na ujenzi wa familia bora.
Kiu yake sio kuwa kituo cha kulelea mwanume au mwanamke aliyeharibiwa na wazazi wake kwenye malezi.
Hatamani kulea mtu ambae hawakufunzwa vyema huko awali alikotoka. Kiu yake sio kuja kuhangaika kubadili tabia mbaya za mtoto wa mtu mwenye meno 32 kama yeye.
Anahitaji mtu atakayemrekebisha na kumfundisha mambo madogo kama vile ustaarabu nk tu na vinginevyo!
Furaha yake ni kuona anapata mwenza wa kusaidiana nae kwenye maisha sio mtu wa kusaidiwa na kurekebishwa tu kwenye kila kitu. Sio jukumu lake Leo kwenye ndoa ndio ahangaike kukufundisha, kukumbuka majukumu yako, akufundishe kuweka akiba ya pesa.
Akufundishe kutumia pesa vizuri, akufundishe usafi, kusali, malezi,na mengine mengi.
Tuingie kwenye ndoa kufurahia na kushiriki maisha pamoja na sio kutumia muda mwingi kulea na kurekebisha. Ndoa sio kituo cha malezi na wala sio gereji.
Watu tujifunze wajibu wetu kabla ya kuingia kwenye ndoa, na kama hujui wajibu wako, ulixa hapa watu watakuelekeza... Kama unaona aibu njoo kwenye huduma zangu za ushauri
...
Ndoa siyo sehemu ya kujifunzia wajibu, umegeuka kero, kuna wengine mnaishi maisha ya kwenye upenzi mpaka kwenye ndoa, dharau dharau, kuchukulia poa hakuna ule utii na heshima ya kumpa mwenzio kua huyu nimmeo huyu nimkeo..
Mambo ya ajabu tu
Watu mbadilike