MAKOSA 7 USIMFANYIE MWANAMKE๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ’”๐Ÿ’”"




1.Usimpige
2.Usimdhalilishe kwa kauli na Matendo
3.Usimvunjie heshima
4.Usimfanye ahisi kuwa hapendwi
5.Usimbake
6.Usimsaliti
7.Usipuuze Lugha zake za Mahaba

"Mpe wema , atakupa Upendo"
"Mpe Tabasamu,atakupa kicheko"
"Mpe Moyo wako,atakupa maisha yake"
"Mpe nyumba ,atakupa makazi na utulivu"
"Mpe wazo, atakupa mipango"
"Aminiana naye kama Malikia wake, Atakufanya kama Mfalme wake"
"Mpende , Atajikabidhi kwako"

"MTHAMINI SANA MWANAMKE ILI AKUONYESHE MAPENZI YAKE YOTE YA KWELI❤️❤️๐Ÿ’"

"NA PIA KWA WANAUME NA WANAWAKE๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ’”❤️๐Ÿ’”๐Ÿ‘‡"

๐Ÿ‘‰MFAHAMU ADUI MKUBWA KATIKA MAHUSIANO๐Ÿ‘‡

Kuna maadui weeeengi wametuzunguka ndani ya ndoa zetu na mahusiano yetu na kama hatukupambana nao hatuwezi kua na utulivu Wa nafsi hata siku moja.

Leo naomba tumuangalie adui namba moja anaitwa
"DHARAU"

DHARAU na KUTOKUJALI ni maadui pacha wanaofuatana,hakuna binadamu anaependa kudharauliwa hata aweje,kila mmoja anahitaji kuona cheo chake kwa mwenzake.

DHARAU ni donda sugu linaloondosha uhai Wa ndoa zetu kila kukicha.

๐Ÿ‘‰Mwenzako amekukataza kitu hujali........
๐Ÿ‘‰Mwenzako amekushauri kitu hujali.......
๐Ÿ‘‰mwenzako anaumwa hujali.....
๐Ÿ‘‰mwenzako amepata matatizo hujali.....
๐Ÿ‘‰mwenzako ameomba umfanyie kitu hujali....
๐Ÿ‘‰mwenzako anaongea nawe hata humuangaliii wala humsikizi......
๐Ÿ‘‰mwenzako anachukia kitu ndio unafanya maksudi....

Hizo ndio DHARAU na kuonesha dharau hata kwa wazazi na ndugu Wa mwenzako.

Tujaribu kuwafukuza kwenye nyumba zetu maadui hawa #DHARAU na #KUTOKUJALI na badala yake tuwakaribishe #KUJALI na #KUBEMBELEZA

Hebu anza kumuonesha mwenzako kua unamjali na unajali hisia zake, anapoongea nawe acha yote mskize kwa umakini hata kama hufurahii analosema ,mshauri kwa lugha ya upole ,muoneshe upendo na tabasamu mda wote, akikosea mfahamishe kistaarabu hakuna mkamilifu hata wewe pia unakosea
@maisha_halisitz
Be smart

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA