MAHUSIANO NA NDOA NYINGI ZA SASA NI SAWA NA NGUO ILOCHAKAA KUTWA UPO KWA FUNDI KUZIBA VIRAKA🤦♂️
Wengi wanatafsiri MAHUSIANO AMA NDOA kama hakika ya kuwa na mtu kwa ajili ya kukamilisha MAHITAJI iwe ki mwili ama ki maisha, badala ya maana halisi kwamba;-

Ubinafsi umekuwa kipaumbele kwa jamii yetu kiasi kwamba kila mmoja anataka apewe nafasi kubwa kuliko mwingine.
Ili upendwe na kupewa thamani kwenye MAPENZI unawajibika kugharamia iwe kwa MALI
AU MWILI



Migogoro imekuwa chakula cha mahusiano na ndoa nyingi kuliko UPENDO hata kupelekea maumivu makubwa kwa kila aliyeamini katika UPENDO 

Kwa sasa ili japo upate FURAHA NA AMANI ya mpito unatakiwa kujipima uwezo wako ki fedha ili wewe utoe pesa na mwingine akupe haja yako



Maana kumpata mtu sahihi ambaye atakuwa nawe kwa MOYO wake unawajibika kuomba rehema za MUNGU ili kumpata huyo, Kwa nadharia ni kama ndo FASHION lakini kumbe MAJERAHA YA MAPENZI YAMEWAJENGA WENGI KUAMINI HAKUNA UPENDO WA DHATI 

Japo najua kabisa MAPENZI YA KWELI BADO YAPO ila tu kuyafikia ni hatua ngumu

Hatuwezi kuyakwepa MAPENZI bali tunawajibika kuyafikia yale ambayo ndiyo ya HISIA zetu halisi, hayo yanaweza kukupa FURAHA NA AMANI YAKO.