ZAO LA UPENDO ❤️ HUSITAWISHWA ZAIDI NA NINI UNAFANYA KWA ALIYEKUPENDA💯
Moyo ni shuhuda wa nini mtu anafanya kwako ikiwa wewe umeamua kumchagua awe wako kwa UPENDO WA DHATI 

Huwezi kupewa UPENDO kama wewe hujaonyesha sauti ya matendo yatokanayo na UPENDO kwani tabia ya NAFSI ni uhakiki wa nini unafanya kulingana na vile NIMEKUPENDA.
Muda Mwingine mtu akipendwa huona kama sheria

Ni kweli MUNGU anaagiza UPENDO kwa wengine ila ni kwa ajili ya UBIN ADAM

Unapozungumzia UPENDO WA MAHUSIANO NA NDOA huo unahitaji MAPOKEO YA MAPENDO unipende nami nikupende bila kujiangalia wewe ni nani ila ni kwa sababu hiyo hiyoooooo kwamba;-

Huwezi kutaka UPENDO halafu mtu akajua unamtumia kwa maslahi yako akabakia na UPENDO HALISI

Kila mara nasema;-

Tafuta kuaminiwa na NAFSI japo moyo ndiyo mjumbe wa UPENDO lakini IMANI YA UPENDO huzaliwa na NAFSI

Tafuta kuwa mwenye FURAHA NA AMANI kwa kulinda IMANI YA UPENDO kwa mwenza wako, Huwezi kuwa na Mtu halafu unataka yeye akupende ila wewe humpendi halafu ukadumu katika UPENDO WA MWINGINE

UPENDO una tabia ya kuambukizana matendo ya UPENDO ni rahisi kuwa katika PENDO IMARA kama hakuna unafiki

Mpende anayekupenda na kuijua THAMANI yako, Kama hujaona UPENDO wake na hujui kama ana thamani uwepo wako kwake PIGA CHINI HARAKA unapoteza muda

Muda Mwingine wanaotuhadaa ni wale wanaotafuta PANADOL baada ya HOMA ZA MAHUSIANO NA NDOA zao, hao ndio wengi kuliko wenye NAFASI PANA MIOYONI MWAO na ukimpata huyo mjenge katika hakika ya UPENDO 
