KUELEZANA UKWELI KWENYE UCHUMBA WENU NI KITU CHA MUHIMU,EBU TUJIFUNZE KWENYE MKASA HUU...


Mwaka fulani kaka mmoja katika kanisa fulani alitaka kuoa,kweli akaanza taratibu za kutafuta mchumba ili hatimaye aweze kuoa..
Kaka huyu alikuwa ni muudhuriaji mzuri wa ibada kweli alikuwa awezi kukosa ibada kizembe , vile vile alikuwa mtanashati sana,mdada awaye yote ni ngumu kumkataa..
Basi akamshirikisha mchungaji wa juu ya swala lake la kuoa mchungaji wake akaampa baraka zote,,basi akachagua dada mmoja katika ilo kanisa na hatimaye wakaanza taratibu zote...
Kweli walifanikiwa kufunga ndoa yao,na baadae baada ya tafrija ya harusi yao wakaambiwa sasa waende nyumbani...
Kilicho washangaza wengi kijana huyu pamoja na utanashati wake alikuwa hana chumba wala nini,sasa akaulizwa kwann umechukua hatua kuoa wakati huna chumba wala mahali popote pakuanzia maisha na mkeo,kijana akawa hana majibu,kumbe kijana alikuwa anaishi kwa rafiki yake na hata kudiriki kumwambia yule binti kule kwa rafiki yake ni kwake na wakisha oana basi rafiki yake yule atawapisha....
Watu wakaishiwa na nguvu ikabidi kanisa liwakodie gest siku mbili baadae kuwapangia chumba,binti yule akaanza kulia kweli,mchungaji akamwambia huyo tayari ni mumeo na hakuna jinsi lazima uvumilie ndo mwanzo wa safari....
Tunajifunza nini ukweli ni silaha bora katika uchumba kuwa mkweli ili mtu ajue anaenda kuishi na mtu wa namna gani kwann unaigiza maisha halafu mtu anakuta maisha yale si halisi...
Kama una mtoto au watoto sema kwa mchumba wako ili ajue mapema,ni mbaya sana kuficha afu ikatokea mpo kwenye ndoa akijua uwe na uhakika ilo ndo anguko la ndoa yenu..
Ukweli umuweka mtu huru acha kuogopa kwamba nikisema ukweli ataniacha ni bora useme ukweli ili mtu afanye uamuzi sahihi,ikitokea amekuacha basi jua moja huyo hakuwa wako....
Yote kwa Yote tukumbuke hizi ni siku za mwisho na Yesu Kristo yu malangoni kuja kunyakua wateule na baada ya hapo inakuja dhiki kuu ambayo haijawai kutokea tanguu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu,mimi na ww tusitamani kuwepo siku hizo mbaya,tuzidi kuutafuta UTAKASO KILA IITWAPO LEO.
May be an image of 3 people, people standing and outdoors

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA