DALILI ZA MIMBA
1. Kuwasha na kuvuta kwa chuchu
Kadiri homoni za mimba zinavyoongeza usafirishaji wa wa damu kwenye matiti yako, unaweza kuhisi hali ya kuvuta kuzunguka chuchu zako. Hii inaweza kuwa moja ya dalili za awali za mimba, na muda mwingine kugundulika pia ndani ya wiki au zaidi ya utungaji wa mimba. Mara baada ya mwili wako kuzoea ongezeko la homoni, hali hii itapotea.
2. Maumivu ya tumbo na kugundua kuchafuka.
Sio kawaida kuchafuka ukiwa na karibia wiki 6 za mimba. Unaweza kugundua rangi ya pinki kwa mbali au madoa ya kahawia katika nguo zako za ndani(chupi) au wakati unakojoa au kuhisi maumivu ya tumbo kwa mbali. Wataalamu hawana uhakika kabisa kwanini dalili hizi zinatokea katika hatua za awali za mimba. Inafikirika kusababishwa na ukuaji wa plasenta. Kama umekumbwa na tatizo la kutokwa damu ambalo sio kawaida, muone daktari mapema ili kuwa katika hali ya usalama.
3. Kujisikia kuumwa.
Kama una bahati utaepuka kichefuchefu kabisa. Hata hivyo,magonjwa ya asubuhi ni moja ya dalili za awali za kawaida za mimba, japo zinaweza kuanza mapema katika wiki ya nne. Unaweza kujisikia kuumwa na kichefuchefu. Hali hii inaweza kukupata mda wowote ndani ya siku, mchana au usiku.
4. Kukua,kuvimba kwa matiti.
Mara baada ya kufika wiki ya sita ya ujauzito wako, matiti yako yanakua nyeti zaidi. Inakua sawa na jinsi unavyojisikia kabla ya hedhi. Unaweza kugundua kwamba maziwa yako yamekua na kuvimba,na mishipa kuonekana chini ya ngozi. Kukua kwa maziwa ni dalili ya kawaida katika miezi mitatu ya kwanza ya mimba.
5. Kujisika kuchoka.
Umechoka? Unaweza jikuta unashinda kitandani mda wote kadiri mwili wako unavyojitahidi kukubaliana na uwepo wa mtoto ndani yako, tangu mwanzo wa mimba. Homoni za mimba za mwili wako ndio zinakufanya kuhisi umechoka, mwenye hasira na hisia kali. Uchovu ni dalili ya kawaida ya mimba, na hutokea zaidi katika kipindi cha kwanza cha mimba na hatua za mwisho