SIFA SABA ZA MKE MJINGA.
1)MKE KING'ANG'ANIZI.
Mke Mwenye Sifa hii ya Kung'ang'ania Kitu,Huwa ni Chukizo na Kero kwa Mume wake na Tishio la Furaha yake,Mke Huyu Kila Akitakacho Hulazimisha Mpaka Akipate Pasi hata ya Kuitazama Hali ya Pato la Mume wake.
Chukua Hili Dada
Asmaa Binti Khaarijah Alimuhusia Binti yake Namna ya Kuishi na Mume Wake.Akasema
"Kuwa Kwake Mume Wako ni Ardhi naye Atakuwa Mbingu na Uwe Kwake Tandiko atakuwa kwako Nguzo,wala #Using'ang'anie Kitu Atakuchukia.."
2)MWENYE HARUFU MBAYA
Mke Huyu Hajishughulishi Katika Kujisafisha wala Kujipamba Kwaajili ya Mume Wake,Basi Sifa yake Kuu ni Kuwa na Hali Chafu ya Mwili na Hata Mavazi yake na Huyu ni Tishio la Utambulisho wa Mume wake Katika Kumtambulisha yeye Kwa Ndugu na Jamaa zake
Chukuwa Hii
"Umaamah Bint Haarith Alimuhusia Binti yake Katika Ndoa yake,Kwamba.
"Jicho lake Mume wako Lisianguke Kwenye Eneo lako Lenye Kuchukiza na Wala Asisikie Kwako Ispokuwa Harufu Nzuri"
3)MWENYE LAWAMA NYINGI.
Hii ni Aina ya Mke Mjinga Ambae Kila Wakati Hufukia Mema na Mazuri ya Mumewe na Hutumia Kutereza Kwake kama Ni Fimbo ya Kukithirisha Lawama Zake.Huyu ni Tishio la Furaha na Haiba ya Mumewe.
Chukuwa Hili Dada.
Swahaba,Abuu Jaafar Bin Abi Twaalib,,Alimuhusia Binti yake,Kuwa.
"..Jihadhari na Lawama Nyingi Kwani Hurithisha Maudhi"
4)HAJALI TUMBO LA MUME WAKE
Mke Huyu Huweka Mbele Furaha ya Macho na Stori na Mashoga zake Mpaka Anasahau kuwa Kuna Mume Anayehitaji Kuandaliwa Kile Kitakacho Ingia Tumboni Kwake na Kuondoa Njaa yake. Hupumbazika na Stori,Tamthilia na Kusahau Njaa ya Mumewe
Dada Lako hili
Umaamah Binti Haarith,Alimuhusia Binti yake Jinsi ya Kuishi na Mume Wake Akasema.
"Angalia kwa Makini Wakati wa Kula kwake na Kulala Kwake Kwa Hakika Njaa Nyingi Huchoma na Kukosesha Usingizi na Hutia Ghadhabu"
5)ASIYE SAMEHE.
Mke Huyu Hulazimisha na Kutaka Mume Wake Adumu Katika Nafasi ya Kuwa Ni Mkosaji Ili Aweze Kumuhesabia Ukosefu wake.
Dada Kumbuka.
Abuu Dardaa Alimshauri Mke Wake Kuwa.
"Samehe Utadumisha Mapenzi yangu.."
6)MWENYE KUMBISHIA MUME WAKE.
Huyu Haambiliki wala Hayuko Tayari Kukosolewa Pale Akoseapo.Acha Hii Tabia.
7)HATAKI KUSHAURIWA.
Huyu Huwenda Ukawa ni Wewe Unayesoma Mafundisho Mengi ya Kumtii Mume Wako Lakini Bado Unafanya Uozo Katika Ndoa yako.
Muu Mata