UNAPOBEBA MIMBA YA MCHUMBA WAKO JUA KUA KUNA MWANAMKE MWINGINE NAYE ATABEBA KUKUKOMOA!
Nirahisi sana kusema wewe beba tu mimba nitahudumia, wadada wengi amabo wananiomba ushauri waliambiwa hivi, lakini wengi mwanaume ligi inamshindia mimba ikifika miezi sita tu. Kama umebeba mimba hajakuoa basi kama ndiyo changa basi jua ikifika miezi sita utashangaa laini zake hazipatikani, lakini kama ndiyo unampango wa kubeba mimba yake basi niishakuambia usije kusumbua watu baadaye atakuja kukutelekezea ikifika miezi sita.
Mwanzoni mwanaume huona nitaweza, lakini nilichogundua nikua vijana wengi wana wanawake zaidi ya mmoja na mara nyingi mmoja akipata mimba utakuta na miwngine anayo na mwingine. Kuna mtu unakuta analalamikiwa na wadada watatu, sasa ndugu yangu mimba tatu kwa wakati mmoja mtu mwneyewe hana kazi au ana kazi na chumba kimoja au chumba na sebule unategemea nini!
Mara nyingi hii hutokea babati mbaya ila akina dada nao wana ujinga huu, akiona boyfriend wake kampa ujauzito mwanamke mwingine basi kimuhemuhe humpanda, anaanza kuona yule mwingine ataolewa hivyo nayeye hutegeshea mimba ilia olewe. Mwingine naye anaona hivyo anategeshea, hapo ndugu yangu lazima mtelekezewe, jamaa anakimbia ajanua kua utaleatu tena ikishafika miezi sita si ndiyo haitoki.
Kwamba mwanaume atakupa moyo sana mwanzoni, anataka mtoto kweli lakini hawezi kulea na akiangalia kwenu mna kauwezo au una kakazi basi atajifanya kukupenda visimu na vingine. Ila dada yangu mimba ikifika miezi sita humuoni, hapo anajua kua huwezi kuitoa hivyo anakutelekezea anasubiri mtoto akifika miaka saba hapo mambo yake yatakua fresh anakuja kumchukua.
Narudia tena dada zangu najua mkishapenda mnajidanganya sana ila wewe jua tu kama hajakuoa basi ukibeba mimba yake atalealea mpaka miezi mitano, miezi sita ni utapambana na hali yako. Sasa wewe badala ya kujifunza kalenda yako na kujifunza kutumia condom nenda kulipia kwa Kugwi kujifunza kukata viuno, utakata lakini jua viuno havinunui uji wa mtoto wala Pampas, utalea mwenyewe na kusumbua ndugu tu!