Mwajiri Wangu Anajua Mimi ni House Girl, Kumbe Mimi ni Mke Mwenzake, House Girl Atoboa Siri.
Kuku wakiwa wengi wanamwaya mtama, kipusa mmoja aliwaacha mashabiki wa radio jambo mdomo wazi, baada ya kufichua siri kuwa yeye sio kijakazi bali mke mwenza.
Kulingana na kipusa huyo mpenzi wake alimpeleka kwake kama kijakazi, ilhali mwajiri wake hajui kwamba ni mke mwenza wake.
Pia alisema kwamba amebarikiwa na mtoto mmoja na mwanaume wa nyumba hiyo, lakini mkewe hajui chochote.
Hii hapa siri yake;
"Nilikuwa na mpenzi licha ya kumkubali, nilifahamu kwamba ana mke, tuliamua anipeleke kwake kama kijakazi, lakini chini ya maji mimi ni mke mwenza
Mwajiri wangu mwanamke hajui kwamba mimi ni mke mwenza, hata amekuwa akiniibia siri kwamba mumewe hana haja na haki ya kitandani
Nina mtoto mmoja na mwajiri wangu na anafanana na watoto wake, ilhali mkewe hajawahi jua kwamba mtoto huyo ni wa mume wake
Aliponiuliza mtoto ni wa nani nilimdanganya kwamba ni wa mwanaume mwingine ili asijue siri yangu na mumewe.
Pia nilimdanganya mwanaume huyo mwingine kwamba mtoto ni wake, na amekuwa akinitumia pesa za kumtunza mtoto wangu
Siku ya jumapili huwa tunaenda na mpenzi wangu kwenye vyumba vya kulala, tunamaliza mambo yetu kisha nina rudi kazini," Alitoboa mwanamke huyo.
Je mwanamke huyo anastahili kutoboa siri hiyo au akanyagie?