MUME, JICHUNGUZE PINDI MKEO ANAPOANZA TABIA HII


Wiki hii nipo na wewe tu mwanamume kwa sababu kwa asilimia kubwa sisi wanaume ndio tunao sababisha migogoro na kutokuwepo kwa utulivu kwenye ndoa zetu,
ni sisi wanaume ndio chanzo kwa asilimia kubwa sana.
Nasema ni sisi wanaume ndio tunaoongoza kuzivuruga ndoa kwa kuwa Mungu alitupa mambo matatu ambayo hakuwapa wake zetu:
*👉1.Utawala*
*👉2.Uongozi*
*👉3.Utukufu.*
Hivyo kwa vyeo hivyo vitatu ambavyo tumepewa na Mungu tulipaswa sisi ndio tuwe mfano wa kuigwa na wake zetu, lakini leo sisi ndio tumekuwa wazinzi wakubwa, walawiti,
wapiga wanawake, wenye maneno machafu,
tusiojua kuongoza wala kutawala,
sisi ndio sababu ya wanawake kuchukia wanaume,
sisi ndio sababu ya wanawake kujaa masokoni, sisi ndio sababu ya kuharibika kwa mambo mengi kwenye familia zetu. Kiukweli Mungu atusamehe na atuongoze.
Yapo mambo mengi ya kujichunguza kila wakati kutokana na namna unavyoishi hapo nyumbani kama baba wa nyumba, ila ukianza kuona mambo haya matatu kwa mkeo,
basi hapo jitafakari kwa haraka zaidi kwa kuwa tayari utakuwa umeshayakanyaga:
*👉1.Pindi mkeo anapokukubalia kila utakalo muagiza, anakuitikia tu "ndio" kwa kila usemacho,*
*rafiki yangu hapo anza kujitafakari. Mkeo hayupo sawa juu yako.*
*👉2.Pindi atakapokuwa haongei chochote mbele yako,*
*hataki stori stori na wewe, ukimuuliza jambo anakujibu kama ulivyo muuliza halafu anakaa zake kimyaa.*
*Hapo jitafakari rafiki yangu*
*👉3.Pindi utakapoona ratiba yake imebadilika ghafla.*
*Ulaji wake umebadilika, ratiba yake ya kulala imebadilika, hapendi tena kuangalia vipindi vya TV anavyo vipendaga, amekuwa mtu wa kufoka foka hovyo,*
*amekua mtu wa mahasira hasira au amekua mtu asie jali tena kuhusu wewe. Hapo rafiki yangu jitafakari,*
*uongee naye, jishushe na myamalize. Vinginevyo yajayo yatakufurahisha zaidi.*
Natumai wote mtakuwa mmeelewa vizuri namna ya kuanza kujitafakari. Usiishi ishi tu bila kujua unayeishi naye ana yepi moyoni mwake kuhusu wewe, wewe sio malaika kwamba siku zote we unapatia tu,
jitafakari.
*Ahsanteni kwa kunisikiliza.*
Follow my page
Share
May be an image of 2 people, beard, people standing and indoor

115
7 comments
5 shares
Like
Comment
Share

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA