USIMHUKUMU KWA KOSA ULILOANZA WEWE KULIFANYA.
Hakuna aliyemkalimilifu chini ya jua,
asiye na hili atakuwa na lile. Na kukoseana au kutenda makosa kwenye mahusiano ni suala la kawaida tena wakati mwingine makoss ndiyo huwafanya watu wapendane zaidi iwapo mkosa atatambua kosa lake na kuacha ujivuni,
Halafu mkosewa naye akatambua thamani ya kuombwa msamaha naye akaacha ukisirani,
hapo kunategemewa mapenzi kati ya watu hawa kuongezeka zaidi na zaidi.
Sasa leo imekuwa kinyume chake, badala ya makosa kuongeza mapenzi,
leo makosa ndiyo yanayoharibu na kuvunja mahusiano ya watu.
Na hii ni kutokana na mkosewa kujiona yeye mkamilifu, na mkosa kutojua maana ya msamaha. Manaake msamaha ili uwe msamaha unapaswa kuwa na sifa tatu:-
1.Kujutia kosa hilo moyoni mwako.
2.Kukiri kosa kwa mkosewa,
3.Kuazimia kutolitenda tena kosa hilo.
Kama msamaha wako utakuwa upo na sifa hizo tatu tutategemea mapenzi kuongezeka zaidi zaidi kwenu nyote.
Ajabu ya leo ni kuwa mume ana mfokea mkewe kwa kosa ambalo yeye mume hulifanya tena na tena,
yawezekana hata mkewe alishamwambia kuhusu kosa hilo lakini mume akalichukulia powa,
ila pindi kosa lile lile ambalo yeye mume alipoambiwa alilichukulia powa linapotendwa na mke ndiyo huzaa ugomvi,
matusi,
vipogo na vikao pia.
Rafiki yangu,
siku zote muosha huoshwa,
Na mganga hugangwa pia. Ubinafsi wetu ni kwamba twajiona sisi ndiyo twaumia zaidi pindi tunapofanyiwa makosa na wake zetu,
lakini pindi sisi tunapowafanyia makosa, tunaomba msamaha kirahisi rahisi tu na tunachukulia powa na tunaona kuwa mkeo hastahili kuumia kwa hako kakosa ulikokafanya. Tuache ubinafsi huo,
hata wao pia wana damu na nyama,
na mioyo yao sio ya chuma.
Mfano,
mume ni mzinifu sana tena sana na inawezekana mkewe alishamwambia hilo suala zaidi ya mara moja na akalipuuzia,
lakini siku akikuta kwenye simu ya mkewe kuna kaujumbe kenye kuashiria mahaba kutoka kwa mwanaume mwingine,
hapo utamuona anavyoghadhibika na kujipa utakatifu asiokuwa nao. Ndugu yangu, Kama unataka mkeo asikuumize, usianze kumuumiza wewe.
Huo ni mfano mmoja kati ya mingi ambayo ipo kwenye jamii zetu.
Kitu cha muhimu kuzingatia kabla ya kuanza kumtolea maneno machafu mkeo juu kosa fulani,
hakikisha hilo kosa wewe hujawahi kumfanyia.
Kwa sababu kumtukana, kumfokea, kumdharirisha, kumpiga, kumuacha na kumnyima huduma mkeo kwa kosa ambalo wewe umeshalifanya, hayo ni matumizi mabaya ya uanaume wako. Kwa kuwa wewe Kama kiongozi wa nyumba ulipaswa kuonyesha njia sahihi ili unaowaongoza waifuate.
Lakini Kama utavuta sigara mbele ya familia yako, usiwahukumu wao watakapoamua kuvuta bangi.
*Natumai umenielewa*