UKIZINGATIA HAYA UNAKWENDA KUTAJIRIKA


Bila kujali una umri gani, una elimu kiwango gani, unapitia magumu kiasi gani amini nachokwambia ukifanya mambo haya utakuwa umefanya Uamuzi Bora maishani mwako-
1. Anzisha Biashara, hakuna mtu aliyetajirika kwa mshahara ama posho labda wale Wakurugenzi wa makampuni makubwa kama CRDB, Amazon, Vodacom, Google, NMB, Microsoft na makampuni mengine makubwa lakini mfanyakazi wa kawaida kamwe usitegemee kutarijirika kwa kupitia mshahara vinginevyo uwe mwizi huko kazini kwako.
Ukiwa bado una nguvu anzisha biashara na jiwekee muda wa kuisimamia ili ikue ili siku ukiacha ama ukikosa ajira ama ukistaafu utakuwa na sehemu inayokuingizia kipato!
2. Wekeza Kwenye Maarifa, Watu wengi wakishahitimu masomo yao hasa ya Chuo Kikuu huwa hawapendi tena kujifunza. Nakushauri uwekeze kwenye maarifa hasa kwa kusoma vitabu, magazeti, majarida, kuhudhuria semina na hata kujifunza humu mitandao kwa watu wenye mawazo chanya ya kukujenga.
Huwezi kuwekeza kwenye Forex, Kilimo ama biashara yoyote ile bila kuwa na maarifa, utafeli vibaya!
3. Tafuta Marafiki Bora, Wengi huwa wanadhani kuwa na marafiki wengi ni sifa---HAPANA, usione aibu kuwapoteza marafiki ambao hawaongezi tija kwenye maisha yako, siyo kila mtu unayejuana nae lazima awe rafiki yako wengine acha wabaki kuwa mnajuana tu. Tafuta marafiki bora ambao watakupa sapoti kwenye biashara yako (nawe utakuwa tayari kuwasapoti) na kukupa changamoto za kufanikiwa.
4. Fuata Moyo Wako, Watu wengi wanafanya biashara na kazi kwa mkumbo. Fanya kazi ama biashara unayoipenda kutoka moyoni mwako, kazi ama biashara ambayo unaipenda na kuijua utaifanya kwa ufanisi kuliko zile kazi ama biashara za 'Show Off' ni heri watu wakucheke unazurula kwa kuuza mchele umejitwisha lakini unaingiza pesa kuliko uwe na duka la nguo linalovutia tukakusifu lakini jioni unafunga huna hata nauli ya kurudia nyumbani
5. Tumia Chini ya Kipato, Hapa ndipo watu wengi wanafeli sana. Kama kipato chako ni TZS 10,000 tumia chini ya hiyo pesa ili uweze kuweka akiba, lakini ukitaka kuonesha umwamba ili sisi tukusifie mwisho wa siku utabaki mwenyewe na njaa zako na sisi hatutakuwepo na hatutajali.
Akiba ndiyo huwapa watu jeuri ya kuwekeza, jifunze kuweka akiba hata kama unapata pesa ndogo kwa siku, wiki ama kwa mwezi. Ukijenga tabia ya kujiwekea akiba ukiwa na pesa ndogo utaweza pia hata siku ukipata fedha nyingi!
Ahsante
May be an image of 1 person, standing and outdoors

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA