MWANAUME MJINGA NI YUPI
Anayebadilika baada ya maisha yake kubadilika kutoka chini kuwa ya hali ya kati au ya juu,kwa maana walianza maisha ya tabu ya dhiki.
Ni mwanaume anayejali watu wengine akadhalau watu wake watoto wake mke wake,familia yake kwa ujumla.
Yupo ladhi kujali familia nyingine kwa kila kitu mke na watoto asiijali kwa hali na mali.
Kisingizio kisiwe na mantiki na walikotoka kabla ajapata kipato alichonacho alijuwa mtu wa kuijali familia yake hata kwa kidogo chake.
Ni mtu asiyeona mchango wa mwanamke wake pale tu alipopata,anasahau walipotoka na anasahau alimvumilia na aliombewa sana kila alipotoka kwenda kutafuta.
Ni mtu anayempe au kuipa nafasi kubwa familia isiyo yake,mwanamke asiye wake,yule anayejifanya kumjali kumpenda kwa sababu tu ana kitu.
Mwanamke aliyempa faraja,aliyemuombea afanikiwe,aliyemvumilia kwa hali yake anamdhalau na kumuona sio kitu.
Familia yako ishindie dagaa na mlenda nyumba ndogo ichague menu ya chakula cha siku.
Hoja ya wanaume et..
Ananipanda kichwani,leo umepata anakushauri mambo mazuri eti anaanza kukutawala,ila zamani alikushauri na ulikubaliana nae.
Anaanza kukufuata fuata,ukiambiwa jambo linaloendana na ukweli unapandwa kichwani.
Hoja dhaifu na ya kijinga.
Hata kama ila kumbuka mlikotoka.
Hata kama ila katu usitese familia yako kisa mchepuko.
Hata kama nje unapewa nini usikubali familia yako ivurugwe na mchepuko kwa sababu mkeo anajua ulikotoka na alikuvumilia huyu mchepuko ajui chochote.
Ukitaka kujua mchepuko upo kwa maslahi,leo ukose pesa,ukose kazi,uumwe.
Ukitaka kujua mchepuko ni shiida rudi maisha ya ulikotoka,maisha yako ya dhiki.
Ndio utajua kati ya mke na mchepuko nani atakufaa,atakufariji na atakayekuthamini.
#MadamKasema