MWANAMKEJUA MAMBO YANAYO HAMASISHA MAHABA KWA MUMEO
1 KITANDA
Mwanamke jitahid kitanda chako kiwe vizur na cha kuvutui kipambe vizur,kwa mashuka mazur yenye nakshi,na shuka inyooke vizur,sio ktanda kinakuwa kama vle stoo ya nguo chafu.
2 MANUKATO
Katka chumba chako jitahid sana,kiwe kinanukia kila Mara mumeo anapo rudi akiingia chumban akutane na harufu nzuri, .sio chumba chanuka jasho na uvundo wa manguo au liharufu lingine lolote la ajabu ajabu👌
3 USAFI
Hili ni jambo la muhimu sana maana utakuta chumbani kuna vichup vya wik nzima, hazijafuliwa mataulo chin,masidiria,mumeo akikuta chumba kiko hivo ujue kuna mwengne atamchukua.
4 Usafi wa mwili
Pia Usaf wa mwili mwanaume anavutiwa na utakavokuwa umejipamba na atavutiwa kimapenzi na wewe. Sio mwanamke kutwanzima na dera moja, kuoga toka ulivyooga jana usiku unasubir tena usiku 👌👌👌 weeehe shoga khoma tena ukomae. MWANAMKE USAFI WA MWILI NI MUHIMU
5 Mapokezi mazuri/Ukarimu kwa mumeo
Wanaume wanapenda sana kupokelewa vizur,kwa MAHABA tele mapokezi utakayo mpa mtu jitahid yawe ya mahaba,legeza macho, mwili,yaan ili mrad tu umchanganye mwanaume Siyo umeshupaa kama mwanajesh kwenye pared🤣🤣👌 anasubir aambiwe nyuma geuka.
6 CHAKULA/MAPOCHOPOCHO/MAAKULI
Jitahid mwanamke kujua kupika sio tu kupika michakula kama ya jela michukuchuku mibaya😥,mamchuz chururu kama watoto wanapika matipwi. Mwanamke kuwa mbunifu mezan kutokana hela ulio achiwa, hata kama si kias kikubwa sana PIKA VTU VIONEKANE VIMEPIKWA👌.
7 MITEGO
Hii ni njia ambayo watakiwa uwe mjanja ukimuona mumeo kakaa seblen basi vaa hata shumiz jipitishe huku ukijitingisha Mara kwa Mara,ujue lazima atakutzama tu tena kwa mwendo nzur wa maringo.
8 MAPENZI
Mapenz ya kumpenda mume pamoja na ndugu zake sio wanapokuja ndugu wa mume unaanza kuvimba kama andazi la kuongezwa
9 UKARIMU NA KUJIPENDEKEZA
Hata kama kwenu ulizoea kuwa na domo kama bakuli la togwa jitahid kuchunga mdomo ukiona huwez mumeo ngoja aondoke ufunge mlango ubwatuke peke yako kaa chiz,akirud funga upuuz wako zungumza maneno mazuri mnyenyekee.