UNAJIKOMOA MWENYEWE MWANAUME HAKOMOLEWI NAMNA HII!
Tatizo la wanawake ni kuwa anaweza kutembea na rafiki yako,
ndugu yako au mtu mwingine ambaye anadhani kuwa anakuzidi kila kitu ili tu kukukomoa,
ili kukuonyesha kuwa anaweza kupata mtu mwingine na kujaribu kukuumiza. Labda niwaambie tu kitu dada zangu, unajitumikisha tu bure,
akili za wanaume hazifanyi hivyo, kama mwanaume kakuacha basi jua kakuacha,
na ingawa anaweza kusikia wivu kidogo lakini wala hawezi kuumia kwa kuwa umetembea na rafiki yake.
Iko hivi mwanaume akishatembea na wewe ujue kuwa kashamaliza mchezo,
kwamba ingemuuma kama ungemkataa yeye halafu ukaenda kumkubali jamaa mwingine ndezindezi hivi, hiyo kweli inauma.
Lakini mtu nishatembea na wewe, nimekuchoka na nimekuacha eti unaenda kutembea na Kaka yangu ili kuniumiza, unajidanganya na kama kwenye akili zenu dada zangu mnajiambia kuwa nimemuumiza au nimemkomoa basi unajidanganya.
Tena kama ni rafiki yake mara nyingi wanaume tunaulizana kabisa.
Kama ni ule urafiki wa karibu utasikia
*“Kile kichwa chako vipi ushakiacha maana naona kinajileta!”*
Basi jamaa anamuambia yule gonga tu hana ishu!
Sasa kama unadhani unamkomoa hapana, sanasana unamhalalishia kuwa afadhali alikuacha kwani heelweki! Sikuambii usitoe huduma kwa rafiki zake wewe toa tu mwili ni wako wala hulipii kodi lakini kama lengo ni kumuumiza basi unajidanganya, anaumia kama alikuwa anakupenda, lakini kama kakuacha yeye halafu ukaenda kujitoa sadaka unachosha tu viungo vyako vya uzazi na si kumuumiza yeye!
*UJUMBE UKUFIKIE WAKURUNGWA*
Follow my page
Share