ANGUKO KUU LA NDOA ZA SASA NI MTU KUMKOSA ALIYEMPENDA KWA DHATI NA KUTAFUTA MBADALA "replacement" ILI KUTIMIZA ADHIMA YAKE


πŸ’―
Siku zote mbadala wa jambo ama kitu huwa sio jibu sahihi, Maana kile kilichotakiwa kuwepo hakipo kwa vyovyote vile HITAJI LIPO PALE PALEπŸ“
Matatizo ya MAHUSIANO NA NDOA za sasa yanaathiri zaidi upande wa Mwanamke kwa sababu kuu moja;-
πŸ‘‰πŸΌ MWANAMKE ANAPOMKOSA MWANAUME ALIYEMCHAGUA MWENYEWE MARA ZOTE HUMKUBARI YEYOTE.
Na ndo maana kwenye ndoa za sasa Wanawake ndo wanakuwa wa kwanza kuchoka na kukinai ndoa, Maana wanawake walio wengi wanaolewa na wanaume REPLACEMENT "mbadala" baada ya wale walowachagua kushindwa kutekeleza shauku yao, Faraja kwa Mwanamke ni zao la MAUMIVU YA KUMKOSA ALIYEMCHAGUA na hapo ndipo Mwanamke kuamua kumchukuwa Mwanaume Mwingine ili atimize haja yake ya kuwa MKE WA MTUπŸ’―
Wanawake walioolewa na wanaume waliowachagua wenyewe always ni WAVUMILIVU na wenye UTII sana, ila ukitaka kujua namaanisha nini jiulize pamoja na mimi;-
πŸ‘‰πŸΌ KWANINI UTII UMEKUWA BIDHAA ADHIMU KWENYE NDOA NYINGIπŸ•ΊπŸ»
Mwanamke akiwa na Mtu ampendaye kwa MOYO hawezi kuwa na dharau wala hawezi kutaka kupambana na mumewe, ila ndoa za REPLACEMENT kamwe AMANI haiwezi kuwa eneo hilo, Zaidi ni majuto pamoja na HASIRA ambazo kama hukuwa timamu unaweza kuharibu ndoto zako, Nini kifanyike kunusuru MAHUSIANO pamoja na NDOA hizi zinazostawi kama uyoga;-
πŸ‘‰πŸΌ MWANAMKE USIKUBARI KUOLEWA NA REPLACEMENT MAANA HITAJI LAKO LITAKUTESA DAIMA.
Kama uliyempenda ameshindwa kukuoa Basi msubiri MUNGU aijue haja yako siku moja UTAPATA HITAJI LAKO ila sio kuona Paulo ameshindwa kukuoa nawe unahaja na ndoa faster unampa nafasi Omari akuoe, niamini Shida yako haikuwa NDOA ila ilikuwa ni wewe uwe na PAULOπŸ“
Kama paulo hayupo niamini Omari sio suruhu ya hitaji lako, tarajia kuendelea kumtafuta PAULO mpaka kufa kwakoπŸ˜‚
Duniani hatuko wawili wawili kwenye hitaji la NAFSI ila tunaweza kuwa wawili wawili machoni kwa kutazamwa ndo maana KULWA na DOTTO hawawezi kupendwa na mtu mmoja ila kila mmoja na mtu wake🎁
Image may contain: 2 people, people standing

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA