MCHUMBA WANGU KANINUNIA KWAKUA NIMEMJULIA HALI BABA WA MTOTO WANGU!




Idd makengo


Habari kaka, mimi ni Mama wa mtoto mmoja, sijaolewa ila nina mchumba ambaye si Baba wa mtoto wangu. Sababu ya kuja kwako kaka nikuwa, huyu mwanaume ana wivu sana, yaanis ijui nikuambieje ananipenda kweli na anahudumia kwa kila kitu, anamhudumia mwanangu kama mtoto wake, lakini shida hataki kabisa niwe na mawasiliano na Baba wa mtoto wangu.

Baba wa mtoto wangu tulishaachana ameoa na ana familia yake. Hanihudumii kwa chochote ila anampenda mt5oto wake na anapenda kunipigia simu kila siku ili kuongea na mtoto wake. Hilo kwake halina shida, hakasiriki yeye kuongea na mtoto wake, lakini shida ni mimi nikitaka kumjulia hali huyo Baba wa mtoto basi yeye hukasirtika.

Mara nyingi najitahidi kutokuongea naye mbele yake, lakini yeye hukagua siimu yangu, akikuta nimempigia anakasirika nimempigia kwanini wakati labda mtoto alikua shule. Kaka nashindwa kuelewa kwani inamaana siruhusiwi kuongea na Baba wa mtoto wangu, sisi ni wazazi, hahudumii wkeli lakini anataka kujua kuhusu mwanae.

Tumekua tukigombana sana lakini kila nikimuelewesha wmanaume wangu haelewi. Sababu ya kuja kwako kaka ni hivi, juzi nilimtumia meseji Baba wa mtoto wangu, nikamuuliza umeamkaje,hakunijibu, basi nikahisi kama kuna tatizo, nikampigia hapokei, nikamtumia mseji nyingine kulalamika kwanini hajibu meseji zangu na hapokei ana tatizo gani.

Basi nilishaau kuzifuta zile meseji, Mchumba wangu akaziona, amekasirika haongei na mimi. Nikimuuliza ananiambia kuwa tupeane nafasi kwani anahisi kuwa simpendi basdo sijamsahau X wangu. Nimejaribu kumuomba msamaha lakini haelewi, kaka naomba nisaidie, hivi huyu mwanaume atakua ananipenda kweli, na je kuna ubaya gani nikimjulia hali Baba wa mtoto wangu?

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA