Sababu 5 kwanini kila mahusiano mapya unaishia kuachwa!

Unajiona kama mtu mwenye laana, kila ukiingia kwenye mahusiano hayakai muda mrefu, mahusiano yako yanakaa miezi miwili au hata hiyo haifiki unaachwa.unajihisi kuchanganyikiwa, unajiona mbaya, unahisi huwezi kupendwa basi hizi zinaweza kuwa ndiyo sababu unaachwa na si hizo zilizopo kichwani kwako.

(1) Unaenda kwa kasi sana kila unapoanzisha mahusiano. Umekutana na mtu, hata hamjajuamna vizuri ushamuambia kila kitu chako, ushaanza kumtambulisha kwa marafiki zako kama mke/mume, ushaanza kutaka kujua kwao, kutaka mfanye vitu pamoja, kuongelea habari za mtoto, unaonyesha mchecheto wa hali ya juu.

Kwa mwanaume ukiwa hivi wanawake wenaweza kukupapatikia na kuona uko siriasi ila ukizidisha sana mwanamke mwenye akilia tajiuliza kwanini una haraka, labda kuna kitu unakificha hivyo kurudi nyuma. Kwa mwanamke ukiwa hivi mwanaume anakuona kama umechanganyikiwa sana kuhusu ndoa, anakuona huna maisha na utamsumbua hivyo kukuacha kwani anahisi utakua mzigo kwake.

(2) Unalalamika sana kuhusu mahusiano yako ya nyuma; Hakuna mtu anyaetaka kusikia kuhusu X wako, hata kama aliuliza anataka kusikia tu mara moja, kama kila siku unazungumzia jinsi ulivyoumizwa, uko na mpenzi mpya badala ya kufurahia mapenzi unaanza mambo ya “Sijui kama nitakuja kupenda tena” basiutaishia kuachwa.

Mpenzi mpya anakata tamaa mapema, anahisi bado unamkumbuka X wako, anahisi ulimpenda sana X wako hivyo utamrudia au huwezi kumpenda yeye tena. Lakini wakati mwingine kujifanya mnyonge kunatia kinyaa, mtu ambaye kila siku analalamika kuachwa achwa anatia kinyaa na kufanya iwe ngumu kupata mtu wa kukushikilia.

(3) Unataka mpenzi wako awe ndiyo kila kitu kwako akutiumizie na mahitaji yako. Kuna watu hawana furaha wakiamini kuwa wakipata wapenzi ndiyow atakua na furaha, kwasababu hii akipata mpenzi nataak kuongea naye kila dakika, anataka kutoka naye kila dakika, anataka akiwa na shida basi mpenzi wake ndiyo awe wakwanza kumsikiliza na kumsiadia.

Awe mpenzi, awe rafiki, awe mtu wa kutoka naye, n ahata mahitaji ya kifedha basi atomize, hasa wanawake, unakuta anaanza kuomba pesa mapema na akiambiwa hapana ananuna na kuhisi mtu hayuko siriasi. Ukweli nikuwa, hakuna mtu wa kukufanyia hivyo, unahitaji marafiki, hobi yako, na kuwa na maisha mengine na wetu wengine bila kumtegemea mpenzi wako.

(4) Unaanza kumpangia mpenzi wako maisha, kumchagulia marafiki na kutaka abadilike ghafla; Una mpenzi wako kichwani, una mambo ulikua unayawaza, labda sitaki mtu wangu anywe pombe, sitaki avae nguo za namna gani, sitaki hiki sitaki kile. Sitaki awe na marafiki, nataka awe anaenda kanizani/msikitini, nataka awe mtu wa familia na vitu kama hivyo.

Basi unaingia naye unaanza kumpangia hayo mambo, unataka ghafla awe kama unavyotaka. Hutaki tena awe na marafiki unataka wewe ndiyo umchagulie unakasirika kabisa na kuwaona kama maadui, ndugu yangu itakula kwako, ingia tayaribu atakuchuka mapema.

(5) Umeshajiaminisha kuwa wewe ni mtu wa kuachwa hivyo wanakuacha kweli; Kuna wale watu, umeachwa mara mbili tatu bais ushaanza kujiambia kuwa mimi nina mikosi, mimi ni mtu wa kuachwa yaani unajitamkia kuachwa kila dakika. Hapa moja kwa moja unajitia gundu mwenyewe lakini pia unakata tamaa mapema.

Ukishajiaminisha hivi basi mtu hata akifanya kakosa kidogo unaona kama ni walewale, kwakua X wako alianza kutokupokea simu akakuacha na huyu naye asipopokea unahisi atakucha unakasirika, unakua na kisirani unajikuta mnaachana. Unamkasirikia kwa kosa dogo kwakua tu na X wako alishakufanyi kosa kama hilo.

Wakati mwingine unakata tamaa mapema, unaona bora nimuache kabla hajaniacha kwakua tu amerfanya kitu kama cha X wako. aise hakuna mtu mwenye laana, laana ipo kichwani kwako, unaweza kuacha na watu kumi ili tu ukutane na mtu wa 11 ambaye ndiyo atakua Baraka kwako, kuachwa si laana ni sehemu ya maisha.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA