Jifunze kuongea maneno mazuri na yenye kushawishi kuliko kulalamika
⌚kuna njia nyingi za kufikisha ujumbe kwa mwenza wako, mtu mmoja anaweza kusema maneno yaleyale yakawa mazuri ila mwingine akayasema na kuwa mabaya, jifunze namna ya kuongea na mwenza wako.
Mfano, mwenza wako anachelewa kurudi, badala ya kumuambia “Kwangu mimi huwezi kunirudia saa nane usiku halafu nikufungulie mlango!” Unaweza kumuambia “Usiku unamambo mengi, kwanini usiwe unawahi kurudi mume wangu, hata ukala kwanza ndiyo ukatoka, kula usiku namna hii sio vizuri!”
Ukamuambia “naomba basi wakati napika unisaidie kusuuza hivyo vyombo ili tule maana nimechoka.” Badala ya kumuambia, yaani hunionei hata huruma nipike, nifue, nioshe vyombo wewe umekaa tu.”
Ni mke wako, umerudi chakula bado, badala ya kuanza kutukana, ongea vizuri “Leo vipi nina njaa, vipi msosi bado…” Umekuja na wageni, ndani kuchafu badala ya kutukana kusema “Mnakaa kaatu hapa hata kufagia ndani huwezi?”
Mwambie “Leo vipi mke wangu, mbona hivi, una nini unajua nakuja na wageni hata hujaparekebisha rekebisha?” Chagua maneno, ujumbe unafika bila kudhalilisha.
Unapoongea maneno mazuri kwa mwenza wako inamfanya kujifunza zaidi na kukupunguzia kisirani, unakua na amani ya nafsi.
#MadamKasema
@maisha_halisitz