Ujinga ni pale ambapo unamchumba mzinzi kila siku unamfumania lakini unakubali kumuoa/kuolewa naye kwa kisingizio kuwa labda atabadilika

Ujinga ni pale ambapo unamchumba mzinzi kila siku unamfumania lakini unakubali kumuoa/kuolewa naye kwa kisingizio kuwa labda atabadilika

 ndugu yangu kubadilika kwake hakuhusiani na wewe, anaweza kubadilika lakini si kwasababu ya ndoa bali kwakua tu kaamua au kakumbwa na kitu flani. Unapokubali kuoa/kuolewa na mtu ambaye kila siku unamfumania basi hakikisha kuwa umekubaliana na hali kuwa hautakua peke yako.


Kuolewa/kuoa mtu wa namna hiyo halafu kila siku unalalamika kuwa unamfumania, ana wanawake wengi basi hicho ni kisirani kwani ulikua unajua kabisa jamaa/mwanamke ni kicheche lakini bado ukaingie. Unataka abadilike, unataka aache kudanga kwani kakuambia viungo vyake vya uzazi vimechoka kufanya hiyo kazi. Kuna kudanganywa ukaingia kwenye ndoa na mtu wa namna hiyo kwamba alijificha.

Lakini kuna kujidanganya kuwa atabadilika wakati yeye hajachoka. Ndugu yangu kama ukimfumania mtu mara ya kwanza ni shetani kamtitia, mara ya pili ni bahati mbaya ila mara ya tatu ni tabia zake, ndivyo alivyo hivyo ni uamuzi wako kukubaliana kuwa ndivyo alivyo utulie na roho yako au kujitoa na si kukubali ndoa halafu unaanza kusumbua watu. Wazazi wamezeeka wanataka kupumzika kila siku wewe ni kuwasumbua eti umemfumania, ndugu yangu huo nao ni UFALA tu!

Na kuna wakati kabisa anaona akubali kuolewa au kukuoa wewe kwa sababu tu ya kuonyesha kumvumilia tabia yake akijua hata. Ndani ya ndoa ataendelea nayo hakutakua na neno hao ndio wale anaoa leo kesho anazini na mwingine ila siku ukichoka sasa ndio utataka kuondoka Kwenye hiyo ndoa too late...
Mimi nimemaliza fanya maamuzi leo
@maisha_halisitz

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA